1
Ee Mwokozi, unilinde na uniongoze kweli, Njia ni matata sana, bila wewe nitaanguka.
Kiitikio
Bwana Yesu, uni’ngoze kwa upole, Nikufuate duniani kila siku, kila saa.
2
Wewe ndiwe Kimbilio kwa wakati wa zoruba, Nawe siogopi kitu, kwako tumaini langu.
3
Kisha siku ya mauti utanifikisha kwako, Nitazame uso wako, na machozi yatakwisha.
