1
HAIFAI kuyasumbukia Mambo yatakayokuwa kesho. Baba yangu anajua yote, Ni vizuri nikumbuke hivyo. Yeye mwenye moyo wa upendo Ananipa yafaayo kweli, Kama sikitiko au shangwe, Na amani yake kila siku.
2
Sikuzote Yu karibu nami, Na neema anapima sawa. Achukua masumbuko yote, Yeye aitwaye Mungu Baba. Kunitunza hivyo kila siku, Mambo hayo ame’tadariki. “Kama siku, kadhalika nguvu!” Ni ahadi niliyoipewa.
3
Mungu, unisaidie tena ’kaa kimya kwako siku zote! Niamini sana Neno lako, ’sipoteze bure nguvu yako! Na katika mambo yote huku Nipokee kwa mikono yako Nguvu na neema ya kutosha, Hata nitakapofika kwako!
