1
MUNGU awabarikie nyote Na awe pamoja nanyi! Awalinde kwa amani! Mungu n’ awe nanyi siku zote!
Kiitikio
Mungu n’ awe nanyi dahari Hata mwisho wenu wa safari! Mungu n’ awe nanyi dahari Hata tuonane huko juu!
2
Mungu wetu awalinde pote Na kuwahifadhi vema Kwa mikono ya rehema! Mungu n’ awe nanyi siku zote!
3
Mungu awaangazie nuru, Na awashibishe sana Kwa fadhili zake Bwana! Mungu n’ awe nanyi siku zote!
4
Mungu awainulie uso! Na wakati wa kuhama Mpelekwe kwa salama! Mungu n’ awe nanyi siku zote!
5
Mungu awabarikie nyote, Awalinde mwe huru, Awaangazie nuru! Awainulie uso wake!
