1
NAMTAFUTA mwana wangu, Mtoto yu wapi leo? Aliyenifurahisha mbele, Ningali ninampenda.
Kiitikio
Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu yu wapi leo? Mwanangu, urudi, ninakutafuta, Mwanangu, mpendwa wangu!
2
Uliyekuwa safi sana Katika utoto wako, Uliichafua roho yako Kwa dhambi na njia mbaya.
3
Ninatamani kukuona Katika usafi tena, Na kukusikia ukiomba Na kumshukuru Yesu.
4
Nitafutie mpotevu Kwa pendo na tumaini! Unisalimie mwana wangu, Ya kwamba ninamngoja!
