1
KATIKA matumaini Kwa Mungu wangu Nakaa katika raha Na utulivu. Na Yeye ni mwamba wangu, Imara sana; Katika dhoruba zote Ananilinda.
2
Mwenyezi ni ngome yangu, Sitatetema; Siwezi kuhofu tena Huzuni, shida. Ikiwa ni vita kali, Sitaogopa; Ni msaidizi wangu Karibu nami.
3
Mahali pa kustarehe Kwa Yesu Kristo; Napata amani, raha, Furaha kubwa. Faraja katika shida, Gizani nuru, Na katika pepo nyingi Bandari nzuri.
