1
NILIPOFIKA Golgotha, Nikaiona huko Neema kubwa kama mto, Neema ya ajabu.
Kiitikio
Neema ya Golgotha Ni kama bahari kubwa, Ne’ma tele na ya milele, Ne’ma ya kutosha!
2
Nilipofika moyo wangu Ulilemewa sana, Sikufahamu bado vema Neema yake kubwa.
3
Nilipoona kwamba Yesu Alichukua dhambi, Neema ikadhihirika, Na moyo ukapona.
4
Mbinguni nitakapofika, Furaha itakuwa Kuimba juu ya neema Milele na milele.
