1
E’ mlinzi, twauliza: “Yesu atakuja lini? Asubuhi ya Sayuni Ni karibu? Tuambie!’’- ‘‘Msafiri, yainue Macho yako, angalia! Asubuhi ni karibu, Usimame, usimame!’’
2
Siku heri ya sabato Ya milele ni karibu, Na dalili yake Yesu Hapo itaonekana. Na rohoni tunaona Nchi nzuri ya ahadi. Asubuhi ni karibu, Na ahadi zatimia.
3
Katika Yerusalemu, Mji mpya wa mbinguni, Yesu atatumiliki Kwa upendo na amani. Baragumu italia, Nasi tutaisikia. Yesu ni karibu sana Kutukaribisha kwake.
