1
Siku mateso yatakapokwisha, Kule mbinguni nitakapofika, Kuwa na Yesu Mwokozi karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.
Kiitikio
Hii ni furaha, na utukufu, Na utukufu, na utukufu, Kuwa na Yesu Mwokozi karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.
2
Kwa maana nimeamini Mwokozi, Nitamusifu daima mbinguni ; Kumutazama kwa macho karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.
3
Ndugu wananingojea mbinguni, Tutafurahi pamoja milele; Yesu akinipokea karibu, Hii ni furaha kupita kipimo.
