1
Mwokozi anaishi, ni hapa duniani; Ni neno la hakika, ni neno la furaha Ananihurumia, ananifurahisha, Aa anaka-a karibu siku zote.
Kiitikio
Mwokozi ni hai, ni hai kwa milele, Anatembea nami kwa safari yangu yote ; Mwokozi ni hai, tayari kuokoa, Na ninajua namna gani? Ni hai moyoni mwangu!
2
Ananipenda kweli na kunichunga sana, Na hata ninachoka, nadumu kumufuata; Katika mambo yote Mwokozi ndiye Bwana, Kufika siku atakaponitwa-a.
3
Nasi Wakristo wote, tusifu sikuzote, Tuimbe Haleluya kwa Kristo na Mufalme; Anapokea wote wanaofika kwake, Hakuna anayependa kama yeye.
