1
Ninangoja asubui, ndiyo siku ya baraka, Siku taabu na huzuni zitakapokwisha pia; Na pamoja na Mwokozi, mbali na dunia hii, Nitashinda kumwabudu kwa milele.
2
Ninangoja utukufu, unanga-a toka mbali, Wa Mwokozi wangu Yesu, ndiye “Nyota ya ’subui” ; Katika mapambazuko nitaona nuru yake, Na usiku utakwisha, taabu, zambi, na kuchoka.
3
Nitangoja Bwana yangu, aliyenikufilia; Tamu ni ahadi yake, “Nitarudi kukuita”. Kuja kwake ni karibu, ndiyo, ni karibu sana, Hamu kwaye inazidi, hamu ya kufika kwake.
