1
Ee Yesu, nataka usafi kwa roho, Nataka uishi daima moyoni; Ondosha sanamu, uchafu wo wote, Na unisafishe nipate usafi.
Kiitikio
Unisaidie sasa kutubu, Ee, unisafishe nipate usafi.
2
Ee Yesu, tazama na unisaidie, Nataka kuishi kwa kukupendeza. Sitaki kufanya mapenzi ya mwili, Ee unisafishe nipate usafi.
3
Ee Yesu, sikia na jibu maombi, Ingia moyoni, unibadilishe; Nataka salama, nataka furaha, Ee unisafishe nipate usafi.
