1
Ninakushukuru, Bwana, kwani uliniokoa; Vile ulinisafisha niwe chombo chako safi.
Kiitikio
Chombo chako, Bwana Yesu, niko mikononi mwako, Unijaze, utumie, kila siku, kila saa.
2
Mimi chombo ’tupu, Bwana, unijaze na baraka; Hivi maji ya uzima yatatoka ndani yangu.
3
Sina nguvu ila yako, ndiyo Roho yako, Mungu; Unijaze na uwezo niwe mushuhuda wako.
4
Mimi chombo cha udongo, utukuzwe ndani yangu; Ulininunua Bwana, niwe kweli mali yako.
