1
Yote kwa Mwokozi wangu, kwaye nguvu yangu yote, Mafikili na matendo, vile siku zangu zote.
Kiitikio
Yote kwa Mwokozi wangu, yote kwaye tu daima; Yote kwa Mwokozi wangu, utukufu na heshima.
2
Hii mikono na migu-u ni kwa kazi yake Yesu; Macho yatazame ju-u, na midomo imusifu.
3
Tangu nilipotazama Yesu kule kwa Kalvari, Vitu vyote vya dunia vilikuwa bule kwami.
4
Ee ajabu kubwa, Yesu, yeye Bwana wa wabwana, Ananipokea kwake na mapendo ya kuzidi!
