1
Ee bendera inatwekwa kututangulia, Tusione woga tena, twende kwa kushinda.
Kiitikio
Bwana Yesu anakuja, tumutazamie, Kwa uwezo wake Yesu atatushindisha.
2
Ee Shetani ni karibu, anatutafuta, Anataka tuanguke, tufe, tupote-e.
3
Tunajua Bwana Yesu ni pamoja nasi ; Tusimame sawasawa na askari wema.
4
Vita kubwa, vita kali iko mbele yetu; Tuwe watu wahodari, twende, tutashinda.
5
Basi, kwa bendera yake tunashikamana; Atutie nguvu yake hata kuja kwake.
