1
Jua la roho ni wewe, Mwokozi, Giza haliko pahali ulipo; Wingu la zambi lisifiche Uso wa Bwana machoni mwangu.
2
Hata kwa saa ya kulala usiku Sitaogopa, wewe ni karibu. Nitapumzika kwa salama Kwani unanitunza daima.
3
Saa ya muchana unanishindisha, Nita-anguka usiponichunga, Uache nuru ya mbinguni Kunionyesha njia ya haki.
4
Uwe karibu nami saa ya kufa, Uniongoze kwa bonde la giza Unifikishe kwako juu, Nione uso wako mbinguni.
