1
Niwa karibu nawe, Ee Mungu wangu, Hata katika taabu niwe karibu; Huu wimbo wangu, Bwana: Niwe karibu nawe, Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu!
2
Ninasafiri hapa, sitakawia; Giza ni duniani, raha haiko; Hata ni hivi, Bwana, niwe karibu nawe, Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu!
3
Hata mateso mengi yananipata, Nitakumbuka hili, una rehema, Na yatanikokota niwe karibu nawe; Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu!
4
Saa nitakapokwenda kwako mbinguni, Nitasahau taabu ya duniani; Ungali wimbo wangu: Niwe karibu nawe, Niwe karibu nawe, Ee Mungu wangu!
