1
Utazame Mwokozi aliyekufa kwawe Ili wewe upate uzima; Utazame kwa pendo atakusa-idia, Usidumu zambini daima.
Kiitikio
Ona, ona Yesu! Utazame Mwokozi aliyekufa kwawe Ili wewe upate uzima.
2
Bwana Yesu alisulibishwa kwa Kalvari Ili sisi tupate wokovu; Na alitukomboa kwa damu yake safi, Kwake yeye tupate uzima.
3
Ee rafiki, Mwokozi anakuita leo, Anataka ufike upesi; Unakawa kwa nini, ufike bila woga, Uondoke katika hatari.
4
Fika sasa, pokea uzima wa milele, Bwana Yesu alituletea; Na kuishi mbinguni ni tumaini letu, Umwamini na hutapotea.
